ZANZIBAR NJEMA.


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, July 8, 2010

habari

URAIS ZANZIBAR: Salmin atua Dodoma na Siri moyoni  Send to a friend
Wednesday, 07 July 2010 22:35
0diggsdigg
Waandishi Wetu

Rais mstaafu wa Zanzibar (SMZ),Dk. Salmin Amour 'Commando'(kushoto), akiwa na Waziri Kiongozi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha (kulia), baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma jana, tayari kwa mkutano mkuu wa CCM, utakaomchagua mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar. Shamsi ni mmoja wa wana CCM wanaowania kuteliwa kwa nafasi hiyo. Picha na Edwin Mjwahuzi

WAKATI hatima ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM inaelekea ukingoni mwishoni mwa wiki hii, makundi ya ushabiki yanahaha kuwapigia debe wagombea watatu ambao ni Dk Ali Mohamed Shein, Dk Ghalib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha.Jana rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Salmin Amour (Komando) aliwasili mjini Dodoma akiwa katika ndege moja na Waziri wa Kiongozi Vuai Nahodha ambaye ni mmoja wa wagombea.
 
Kwa muda mrefu sasa Dk Salmin haudhurii mikutana na vikao vya chama kutokana na kusumbuliwa na macho, hali inayoonyesha kuwa hatua ya sasa ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM ina unyeti wake.

Makundi hayo yameunda ushindani mkubwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM itakayofanyika kesho, mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka Dodoma wakati wajumbe na wagombea wanaendelea kuwasili, kuna mchuano mkali miongoni mwa makundi ya wapambe wao.
Fununu zaidi kutoka muongoni mwa wajumbe wa CCM zinasema kuna utofuati kati ya wajumbe wa Zanzibar na wa Bara kuhusu uungwaji mkono wa wagombea hao.
Uchunguzi umebaini kwamba, wafuasi wa vigogo hao wamekuwa wakitambiana na kuelekeza kampeni kwa wajumbe wa Halmashauri ya CCM (Nec), ambao ndio watakaopiga kura kumchagua mtu mmoja atakayeshindana na wapinzani katika kinyang'anyiro hicho.

Taarifa zinaeleza kuwa ingawa Dk Bilal anatajwa kuwa mshindani mkubwa katika kinyang'anyiro hicho, nafasi yake kuingia tatu bora ina utata kutoka na tuhuma za wafuasi wake kuendeleza kutoa lugha isiyonzuri. 

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amedokeza kuwa katika uteuzi huo chama hakitafanya makosa kwa kumteua mtu ambaye watu watamguna na kugoma kumchagua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Makamba alisema Kamati Kuu ya CCM itakutana kesho sambamba na Halmashauri Kuu ambayo itaanza kikao mara baada ya kumaliza kamati ili kuzuia kuvuja kwa maamuzi yaliyofikiwa.

Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC1 juzi, Makamba alisema mgombea urais wa Zanzibar atapatikana kwa sifa zake na jinsi atakavyojieleza mwenyewe mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu (Nec). 

"Hapa hakuna cha mgombea kupita kwa kupigiwa debe wala nini, CCM haiwezi kufanya makosa katika hili kwa kuwa tukimpitisha asiyefaa, watu wataguna na wakiguna ina maana tutashindwa katika uchaguzi; hivyo mgombea atapatikana kupitia sifa tulizozianisha na atakavyojieleza,"alisema Makamba. 

Hata hivyo wakati Makamba akitoa kauli hiyo juzi asubuhi, wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa walisema kulingana na mfumo wa utawala uliopo nchini, rais hawezi kutoka nje ya Baraza la Mawaziri.

Wasomi hao waliwatabiria kwamba, Dk Shein, Vuai na Bilal kuwa ndio wenye nafasi kubwa ya kuteuliwa na Kamati Kuu.
Hata hivyo, walionya kuwa kulingana na siasa za visiwa vya Zanzibar, anahitajika kiongozi imara atakayeweza kuimarisha mshikamano baina ya Wazanzibari.

Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Siasa ya Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema CCM inakabiliwa na changamoto kubwa na kwamba kati ya waliojitokeza kutaka kuteuliwa wapo ambao hawaaminiki kutokana na rekodi na misimamo yao katika uongozi.

"Lakini katika kinyang'anyiro hiki natoa nafasi kwa Dk Shein, Vuai na Dk Bilal," alisema Ally.

Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostine alisema Zanzibar wamezoea michuano mikali ya kisiasa na kwamba, si mara ya kwanza kujitokeza wagombea wengi katika nafasi hiyo.
"Mtu ambaye hakuhusika katika mitafaruku hiyo ni Dk Shein na inaonekana ataweza kuwaunganisha Wazanzibari na hata maamuzi ya kumteua yanaweza yasiwagawe Wazanzibari," alisema Profesa Baregu na kuongeza:

"Pia Dk Shein hayuko kwenye kambi ya akina Karume wala Dk Salmini, au CCM Asilia na CCM Mtandao, hivyo haya ni mambo yatakayomfanya achaguliwe," alisema Profesa Baregu.

Mhadhiri wa Sheria wa UDSM, Dk Sengondo Mvungi alisema idadi kubwa ya wanaowania urais wa Zanzibar imeonyesha kiwango cha juu cha uelewa wao wa katiba ya nchi na haki zao.

Mwenyekiti mwenza wa Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia (Redet), Dk Benson Bana alisema: "Kwanza tuwapongeze tu wametambua haki yao na wameonyesha ukomavu wa demokrasia."

Wanachama 11 waliojitokeza kuwania urais kumrithi Amani Abeid Karume ambaye amemaliza muda wake ni Nahodha, Ali Juma Shamhuna, Dk Shein, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud na Dk Gharib Bilal.

Wengine ni balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, Hamad Bakari Mshindo, Omar Sheha Mussa, Mohamed Yusuf Mshamba na Mohamed Raza Dharamsi.

Wachambuzi wengine wa siasa wanasema sio rahisi kwa Haroun na Shamsi kuingia wote katika tatu bora kwa vile wanatoka katika jimbo moja la Makunduchi.
Ali Karume ambaye ni mdogo wa Rais Amani Karume amekuwa akitamba kwamba, kutokana na elimu yake na uzoefu katika siasa, ana nafasi kubwa ya kuteuliwa na chama chake kama vigezo vilivyowekwa na vitafuatwa.
 
Mohammed Aboud ambaye katika kikao cha kamati maalumu kilichofanyika Zanzibar wiki iliyopita kilimjadili na baadhi ya wajumbe kutoa tuhuma za kughushi vyeti, amekuwa akijitetea kuwa madai hayo hayana msingi na kuwa yuko tayari kutoa ufafanuzi mbele ya vikao vya juu vya chama vyenye maamuzi ya mwisho.
 
Mohammed Raza amelalamikia kutoalikwa katika kikao cha CC kinachofanyika kesho na kudai kwamba kutoonekana kwake Dodoma hakumaanishi kujitoa katika kinyanganyiro hicho.
 
"Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM nilikwenda katika ofisi zetu za chama kutaka ufafanuzi nikaelezwa niende katika ofisi ya masjala ili kupata utaratibu zaidi kuhusu kwenda katika kikao cha NEC Dodoma," anasema Raza katika barua yake kwa Rais Kikwete.

Dk  Salmin akilitua mjini Dodoma saa 8:10 kwa ndege ya Shrika la Ndege la Precision akiwa ameongzana na mgombea wa Urais, Nahodha pamoja na Asha Abdalah Juma ambaye ni Waziri na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala bora, Ramadhani Abdalah, baadhi ya wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Komandoo Salmin, alikuwa wa kwanza kushuka na kufuatiwa na Nahodha na viongozi mbali mbali wa serikali na CCM walifika kuwalaki.
Mgombea mwingine wa Urais wa Zanzibar, Dk Shein aliwasili jana majira ya saa tano asubuhi akifuatiwa na mgombea mwingine, Mohamed Aboud ambaye ni Naibu Waziri wa Afrika ya Mashariki.

Hata hivyo hadi jana mchana ilikuwa haijafahamika kama Bilal amefika Dodoma ingawa wapiga kampeni wake wameuteka mji wa Dodoma.
 
Wakati viongozi hao wakitua, makundi ya wapiga kampeni wa Urais wa Zanzibar kutoka maskani mbali mbali, wamewasili mjini hapa tangu juzi usiku na jana walikuwa wametanda ofisi za CCM na kwenye nyumba za kulala wageni.
 
Wengi wa makada hao wa CCM kutoka Zanzibar walikuwa ni Gharib Bilal toka maskani za mikoa mitano Zanzibar wakiongozwa na wajumbe wa maskani kubwa ya Kisonge, ambao walionya kuwa kamwe hawatakubali kusikia vikao vya juu ya CCM vimemwengua.
 
Kada maarufu wa CCM Zanzibar na mmoja wa waasisi ya jumuiya ya vijana wa Afro-Shiraz, Baraka Mohamed Shamte, alisema chaguo la Wazanzibar wote ni Bilal na kama CCM Bara ikilazimisha kumleta mwingine kitakachotokea watajuta.
 
Shamte alikuwa Katibu wa CCM katika wilaya mbali mbali, ikiwepo Wete Pemba, Unguja Mjini na Pangani mkoani Tanga, kabla ya kurejea Zanzibar.
 
"Tangu mwaka 2000 chaguo la Wazanzibari ni Bilal na hadi sasa na kama wanataka CCM iendelee kuwepo Zanzibar waturejeshee Bilal kuwa mgombea wa Urais,"alisema Shamte.
 
Wajumbe wengine, Ally Mzee na Mohamed Issa Ramadhani ambao walisema wanajua CCM bara wanamtaka Makamu wa Rais, Dk Shein, lakini wajuwe Zanzibar wanamtaka Bilal au Nahodha.
 
Kada Mwingine wa CCM toka Zanzibar, Jamal Ramadhani ambaye alikuwa anaongoza ujumbe wa watu 200 toka Zanzibar alisema, CCM isifanye mzaha katika suala la uteuzi wa mgombea wa Urais Zanzibar.
 
Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Zanzibar, Vual Alli Vuai alimweleza mwandishi wa habari hizi mara baada ya kufika jana kuwa kamati maalum iliyopitia majina ya wagombea Zanzibar imemaliza kazi yake sasa imebaki kazi ya CC na Halmashauri Kuu.
 Habari hii imeandaliwa na Salma Said, Zanzibar, Mussa Juma, Dodoma,
Sadick Mtulya na Salim Said, Dar


Tuesday, July 6, 2010

URAIS ZANZIBAR

Haroun: Mimi ni Obama wa Z'bar

na Mwandishi wetu

 
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Haroun Suleiman ambaye ni mmoja kati ya vigogo 11 waliowania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwania urais visiwani humo, amesisitiza kuwa asitengwe kwa rangi aliyonayo kama alivyotengwa Rais wa Marekani, Barrack Obama wakati wa kampeni zake.
Haroun ambaye ni mmoja kati ya maombaji watano waliopendekezwa na Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano yake na Tanzania Daima Jumatano.
Alisema baadhi ya wapinzani wake kisiasa wamekuwa wakitumia kigezo cha rangi aliyonayo kwamba hastahili kuwa Rais wa Zanzibar.
"Mimi najilinganisha na Rais Obama; Obama alibaguliwa sana kwa rangi yake nyeusi. Lakini wamesahau kwamba alishika nafasi nyingi kisiasa kabla ya kuwa Rais na hakuna aliyehoji rangi yake.
Mimi pia nimeshika nafasi nyingi hadi sasa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kwa miaka tisa, lakini hakuna aliyehoji rangi yangu, leo nawania urais, hoja ya rangi inaibuliwa," alisema.
Kwa mujibu wa mgombea huyo, Wanzibari wanapaswa kumhukumu kwa utendaji wake wa kazi uliotukuka, lakini si kwa kigezo cha rangi kwani amezaliwa hivyo.
Haroun aliahidi kuwa endapo atakuwa rais, ataendeleza harakati za msingi za uchumi zilizoanzishwa na Rais Aman Abeid Karume ili kuufanya uchumi Zanzibar ukue kwa kasi ya kupaa.
Kwenye sekta ya michezo, Waziri huyo aliahidi kujenga viwanja vitatu vipya vya kisasa ili sekta ya michezo iwe sehemu ya ajira kwa vijana na kuchangia uchimi wa taifa hilo.


HABARI

Dk. Shein kitanzani
•  Wapinzani wake wamkamia kumg'oa Dodoma

na Mwandishi wetu

 
KINYANG'ANYIRO cha uteuzi wa urais Zanzibar, kimeingia katika hatua mpya baada ya kuwapo mkakati wa kutaka kumwengua Dk. Ali Mohamed Shein kwa madai kuwa hana sifa.
Mkakati huo ambao Tanzania Daima Jumatano imeunasa, unaandaliwa na kundi la wapinzani wake kisiasa katika kuwania kiti hicho ambapo harakati zake wiki hii zimehamia mjini Dodoma kutakakofanyika vikao vya uteuzi.
Tayari wapambe na mashabiki wa wagombea 11 wanaowania uteuzi wa kiti cha urais visiwani Zanzibar kinachoshikiliwa na Rais Aman Abeid Karume, wamewasili mjini Dodoma kuwapigia debe wagombea wao mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC).
Duru za siasa kutoka mjini Zanzibar na Dodoma kwa nyakati tofauti, zimethibitisha kwamba wapinzani wa Dk. Shein anayepewa nafasi kubwa kutokana na kuungwa mkono na vigogo wa serikali, wamekamia kutumia sheria ya Katiba ya Zanzibar kumuengua kwenye kinyang'anyiro hicho.
Vyanzo vyetu vya habari vilisisitiza kuwa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 1984, ndiyo itakayotumika kumbana Makamu huyu wa Rais wa Muungano.
Kwa mujibu wa Katiba hiyo toleo la mwaka 2003, iliyopitishwa Julai 17, sura ya 15, kifungu cha pili kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa Rais wa Zanzibar.
Kifungu hicho chenye sehemu (a) hadi (d), kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa rais wa Zanziabr kuwa ni pamoja na kuwa Mzanzibari wa kuzaliwa, awe ameshatimiza umri wa miaka 40.
Sifa nyingine ni kwamba awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na sifa ya mwisho inamtaka awe mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa 1992.
"Katika kifungu cha 2(C), kinachosema awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ndicho kitakachotumika kumbana Dk. Shein maana hana sifa hiyo," alisema mmoja wa makada wa CCM.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na kwamba awe Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 21.
Sifa nyingine ambayo wapinzani wa Dk. Shein wamejipanga kumnyuka nayo ni ile ya kifungu cha 68(b) ambacho kinasema awe amejiandikisha au ana sifa za kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
Kifungo hicho kinadaiwa kinaweza kuwa kitanzi kwa Dk. Shein kwani hakujiandikisha katika jimbo lake la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
"Kwa hiyo, Dk. Shein ana mtihani mzito wa kuteuliwa maana hakujiandikisha katika jimbo lake kama mpiga kura. Amekiweka chama na yeye mwenyewe kwenye wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi," alisema mmoja wa wajumbe wa NEC ya CCM.
Hata hivyo kifungu hicho cha Katiba kimewagawa baadhi ya wana-CCM hasa wanaomwunga mkono Dk. Shein kwamba hawezi kubanwa nacho.
Mmoja wa watetezi wa Dk. Shein ambaye ni mjumbe wa NEC, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa Dk. Shein hawezi kubanwa na kifungu hicho na wanaopanga kumwekea pingamizi, wameshindwa kukisoma na kukielewa vizuri.
"Waambie wasome vizuri kifungu hicho na hata nyie waandishi wasaidieni. Hicho kifungu kinasema awe amejiandikisha au na sifa ya kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
"Kwa hiyo, kama hakujiandikisha kupiga kura katika jimbo lake, haina maana kwamba hana sifa maana kifungu kinasema awe amejiandikisha au awe na sifa ya kujiandikisha. Sifa za mtu kujiandikisha zipo na Dk. Shein anazo, hivyo hakuna kibano hapa ila watu hawajui kukitafsiri kifungu hicho cha Katiba," alisema kada huyo.
Wakati wapinzani wake wakijipanga kumnyuka kwa kutumia kifungu hicho cha sheria, Dk. Shein tayari alishaeleza mara mbili juu ya kifungu hicho ambapo mara ya mwisho alijieleza kwenye kikao cha Kamati Maalum ya CCM, Zanzibar.
Tatizo la Dk. Shein linafanana na lile lililowahi kumkuta Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ambapo mwaka 2007 alizuiliwa na sheha kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura kwa madai kuwa alikuwa hana makazi maalum.
Endapo Maalim Seif angeshindwa kujiandisha, wapinzani wake kisiasa walipanga kutumia Katiba ya Zanzibar kumuengua kwenye kuwania kiti cha urais. Hata hivyo Maalim aliruhusiwa kujiandikisha.
Katika harua nyingine, wapambe wa waliomba uteuzi kuwania urais Zanzibar, wako mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya juu vya maamuzi vinavyotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii, mjini Dodoma.
Kama ilivyo ada ya mkutano mkuu wa CCM, mji wa Dodoma umefurika wapambe wa wagombea ambao wamekuwa wakikesha kupiga kampeni.
Tayari makada watano kati ya 11, walioomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais Zanzibar, wamependekezwa kwa kupewa alama za juu na kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Waliopendekezwa ni pamoja na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein, Naibu Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Haroun Ali Suleiman.
Wagombea wengine ni Balozi Ali Karume, Hamad Mshindo, Mohammed Yusuf Mshamba, Mohammed Aboud, Mohamed Raza na Mussa Omar Sheha


Thursday, July 1, 2010

kumradhi

Tunwaomba samahani sana ndugu zetu kutokana na matatizo ya kiufundi leo blog yetu ina tatizo la kuchanganya habari lakini tunalishughulikia kwa haraka, ahsanteni sana. Siku njema kwa wote.

kutoka magazetini

Zanzibar yapata kocha mzungu

Kocha Stewart John Hall kutoka England akiongea na waandishi wa habari.

Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kimepata kocha kutoka England, Stewart John Hall, atakayeifundisha timu ya taifa ya visiwa hivyo, Zanzibar Herous.

Akizungumza jana, Rais wa ZFA, Ali Fereji Tamim, alisema kuwa kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitano na atasaidiwa na makocha wazalendo, Hemed Morocco na Ally Kidi

Alisema kuwa ZFA, kwa kushirikiana na kampuni za Future Century na Global Scouting Beural (GSB), wamefanikisha kumpata kocha huyo na kwamba taasisi hizo ndizo zitakazokuwa na jukumu la kumlipa mshahara.

Mwenyekiti Mtendaji wa Future Century, Hellen Masanja, alisema kuwa licha ya kampuni yake kujishughulisha na masuala ya ujenzi, wameamua kusaidia kupatikana kwa kocha huyo ili kusaidia kuinua na kuendeleza soka la Zanzibar.

Kocha Hall alisema kuwa ameandaa programu za muda mrefu na mfupi kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo na kwamba, anahitaji ushirikiano wa Wazanzibar wote ili wafikie malengo.

Taarifa za Hall zinaonyesha kwamba, ana leseni ya ukocha inayotambuliwa na UEFA ya daraja la kwanza na ya soka la kulipwa, leseni ya ukurugenzi wa vituo vya soka na pia miongoni mwa mafanikio yake, ni kuipeleka timu ya St Vicent & Gernadines ya Vijana wa Chini ya Miaka 20 katika fainali za michuano ya Concacaf mwaka 2008.

Hall amewahi vilevile kuwa mkurugenzi msaidizi wa kituo cha timu ya vijana (U-17 na U-19) ya Birmingham City ya England kati ya mwaka 1998 na 2003.

CHANZO: NIPASHE


Wazee wote kulipwa pesa ya kujikimu Send to a friend
Thursday, 01 July 2010 09:27
Aziza Athuman na Minael Msuya
SERIKALI iko katika hatua za mwisho kutekeleza majaribio ya mpango wa pensheni kwa wazee wote nchini ili kuwazezesha kujikimu mahitaji yao muhimu ya kila siku.
 
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti wa Mpango wa Pensheni kwa Wazee Wote. 
 
"Tanzania sio nchi tajiri, lakini serikali tumeona hatushindwi kuwahudumia wazee kwa kuwapa fedha za kijikimu kwa kipindi tutakachokuwa tumekipanga. Tunaamini uendelevu katika kuwapa fedha hizi kutawawezesha hata wale wanaoishi vijijini bila kujali wataweza kufurahia mazingira wanayoishi na kutambua mchango wao katika nchi yao," alisema Kapuya. 
 
Kapuya alisema serikali kwa kushirikiana na wabia mbalimbali katika maendeleo inafanya tafiti mbalimbali ili kuona namna ya kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii, kuwafikia wananchi wengi ikiwa ni pamoja na wazee.
"Ripoti ninayoizindua leo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kutimiza azma ya kupanua wigo kwa kutoa hifadhi katika jamii yetu, taarifa hii ambayo imekuwa na mapendekezo kadha wa kadha imeifanya serikali kuona kuwa hakuna sababu ya kusuburi tafiti nyingine bali kuifanyia kazi," alisema Kapuya.
 
"Ili kuthibitisha hilo kwa sasa serikali yetu iko katika hatua za mwisho kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Uingereza na tutahakikisha kuwa mara baada ya mazungumzo kukamilika, utekelezaji wake utaanza kwa kutoa pensheni kwa wazee wote," alisema Kapuya.
 
Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee wapatao milioni mbili ambayo ni sawa na asilimia nne ya wananchi wote na kuwa wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.
 
Alisema serikali imeamua kutilia maanani utafiti huo ili kuangalia uwezekano wa kuwapatia pensheni wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea bila kujali kuwa  walikuwa watumishi serikalini na kwamba lengo ni kuwawezesha kupata mahitaji muhimu.
 
"Kuna idadi ndogo ya watu wanaofaidika na utaratibu wa hifadhi ya jamii ambao ni chini ya asilimia nne ya nguvu kazi. Idadi hii ndogo inatokana na kukua kwa sekta isiyo rasmi na kukosekana kwa sheria na mipango ya kuwajumuisha watu walio katika sekta isiyo rasmi," alisema.
 
Alisema kuwa taarifa ya utafiti inaonyesha kuwa mfumo wa asili ya hifadhi ambao kwa miaka mingi umekuwa ukitumika kuwapatia mahitaji muhimu wazee, unadhoofika kwa kasi na kuwaacha wengi pasipo kinga yoyote.
Kapuya alisema watumishi wa umma wamekuwa wakiendeleza vitendo vya ufisadi mara baada ya muda wao wa kustaafu kukaribia kwa kuwa wamekuwa hawana uhakika wa kuishi baada ya kustaafu.
 
"Ufisadi umekuwa ukifanyika kwa watunishi wa umma wakati ambaho aliyekaribia kustaafu anakuwa hana uhakika wa kuishi baada ya kustaafu, hata wengine wamediriki kupunguza umri wakati kipindi chake cha kustaafu kinapokaribia. Na hii tunaishuhudia, unaweza ukaona mzee kaishiwa nguvu lakini haachii kazi kwa vijana," alisema Kapuya.
Vilevile alisema ipo mifuko mitano ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa ikitumika katika masuala ya pensheni kwa sekta mbalimbali za serikali na sekta binafsi ambayo ni NSSF, PPF, PSPF,  LAPF, NHIF na GEPF, lakini akasema haitoshi.
 
Aliongeza kuwa serikali imeanza kuongeza mipango ya utekelezaji wa huduma kwa jamii kwa kupitia Tasaf, Mpango wa Misaada kwa walemavu (PWDs) na Mfuko wa misaada kwa watoto waishi katika mazingira magumu ili kuhakikisha makundi yenye mahitaji muhimu yanafikiwa.
 
Awali akiwasilisha ripoti Mtafiti kutoka Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wazee (Help Age International), Stephen Barrett alisema asilimia 75 wa wazee walioofikia miaka 60 na kuendelea wamekuwa wakiendelea kufanya kazi kulingana na umasikini wa familia zao.
 
Alisema kulingana na mahitaji ya uzeeni wazee wamekuwa wakipoteza uhai wao mapema kwa kukosa mahitaji muhimu na maisha yao yamekuwa yakikabiliwa na magonjwa sugu yanayohitaji uangalizi mkubwa.
"Kuna haja ya serikali kuangalia umri wa wazee ambao hata baada ya miaka 60 wamekuwa wakiendelea kufanya kazi ili waweze kupata mahitaji yao muhimu kulingana na umasikini wao, ili kuweza kuepuka kuwapoteza wazee ambao ni hazina kwa kizazi kijacho," alisema Barrett.
 
Katika hatua nyingine wazee waliwasilisha mada yao, wakiishukuru serikali kufikia hatua hiyo kwa kuwa wazee wamekuwa waathirika wakubwa kwa kubeba mzigo wa kulea yatima wanaoachwa na wazazi wao kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
 
"Asilimia 50 ya watoto yatima hapa nchini wamekuwa wakilelewa na wazee, wakati wazee wanahitaji nao kulelewa, huu mzigo sio wetu. Lakini kwa kuanzisha pensheni kwa wazee kutakuwa na nafuu kubwa ya kuweza kuwalea wajukuu wetu," alisema mtoa mada, Mama Kokupima.

Seif: Nitatimiza ndoto ya Karume  Send to a friend

Thursday, 01 July 2010 09:29

Salim Said
KATIBU mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ametangaza vipaumbele 10 katika uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Zanzibar, akisema kuwa anakusudia kuifikisha Zanzibar kule alikokusudia muasisi wa taifa hilo, Hayati Abeid Aman Karume.
 
Katika taarifa yake ya shukrani kwa wanachama wa CUF iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, Maalim Seif alisema kuwa mambo hayo kumi yatakuwa chachu muhimu katika kuhakikisha kuwa Zanzibar inafikia kule ambako Hayati Karume alikusudia.
 
"Mambo haya pia yatakuwa msingi wa ilani ya uchaguzi ya CUF kwa upande wa Zanzibar," alisema Maalim Seif.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni kuyaendeleza maridhiano ya kisiasa waliyoyaasisi pamoja na Rais Karume ambayo alisema ni njia sahihi ya kujenga umoja wa kweli miongoni mwa Wazanzibari, kuendeleza amani na utulivu uliopo kwa kufuata misingi ya ukweli na mapatano; kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuimarisha Muungano.
"La nne ni kujenga uchumi imara kwa kuzingatia mfumo wa soko huria unaotoa fursa ya ushiriki kwa wananchi wote utakaoratibiwa vyema na serikali, ili kuhakikisha wananchi wanafaidika na fursa hizo na kunyanyua hali zao za maisha katika hali ya neema na tija kwa wote," alisema Seif.
 
Alisema serikali yake itaimarisha nidhamu ya utendaji kazi serikalini na ubora wa huduma zinazotolewa na watumishi wa umma, kwa kusimamia ipasavyo kanuni za kazi, kuwapatia mafunzo ya kazi na kuwaongezea mishahara wafanyakazi, ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kuwa mfano kwa umma.
 
Maalim Seif alisema serikali yake itafuata mfumo wa uchumi wa soko huria, kuirudisha Zanzibar katika hadhi yake ya kituo kikuu cha biashara na huduma katika eneo lote la Afrika Mashariki, kuvutia  uwekezaji mkubwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha bandari na viwanja vya ndege.
 
Alitaja mambo mengine kuwa ni kuendeleza kilimo na kukirejeshea hadhi yake; kuweka msukumo maalum katika kuinua viwango vya elimu katika shule zetu za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu, kuinua na kuimarisha huduma za afya katika hospitali, zahanati na vituo vya afya na kurejesha maadili mema ya Wazanzibari kwa kuhuisha mila, silka na utamaduni wetu na kuwarejeshea wazanzibari hadhi na fahari yao iliyotokana. 
Alisema ana uhakika kuwa CUF itaibuka mshindi katika uchaguzi huo baada ya mazingira ya uchaguzi kurekebishwa.
 
"Maridhiano ya Wazanzibari yaliyoanzishwa na rais wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume, na mimi Novemba 5, 2009, yamebadilisha kabisa sura na mahusiano ya kisiasa baina ya wananchi wa Zanzibar na hasa wafuasi wa CUF na CCM," alisema Maalim Seif. 
Alisema kuna uwezekano wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa uliopangwa kufanyika Oktoba 2010, kufanyika katika mazingira ya uhuru, haki na uwazi. 
 
"Rais Karume amekuwa akisisitiza mara kadhaa kwamba hilo ndilo lengo lake na la serikali yake kuona uchaguzi wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki, ambao utawafanya washindani wote waridhike na kusiwepo na malalamiko yoyote ukiondoa yale yanayotokana na makosa ya kibinadamu," alisema Maalim Seif.
Maalim Seif, ambaye amegombea nafasi hiyo mara tatu bila ya mafanikio, alisisitiza kuwa "imani yangu ni kwamba Rais Karume ataisimamia kauli hiyo kwa vitendo".
 
"Hivyo basi, naamini katika mazingira hayo na tukishirikiana wanachama wote wa CUF kufanya kampeni kabambe za kisasa na za kistaarabu, hapana sababu kwa nini tusishinde uchaguzi huu na kuiongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar," alisema maalim Seif.
 
Alisema utofauti mwingine wa mazingira ya uchaguzi wa mwaka huu ni kwamba, matokeo yake yataifanya Zanzibar kuanzisha muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa. 
 
"Najua kuwa hili litategemea maamuzi ya wananchi katika kura ya maoni itakayofanyika Zanzibar  Julai 31, 2010, lakini mimi naamini kabisa Wazanzibari wamechoshwa na hali ya magomvi, chuki na uhasama, iliyodumu kwa miaka 50 sasa, hivyo basi kwa umoja wao na kwa asilimia kubwa sana watapiga kura ya ndio kuridhia muundo huo mpya wa serikali," alisema Maalim Seif.
 
Maalim Seif alitaja mambo 10 ambayo yatakuwa msingi wa uongozi wake iwapo atafanikiwa kuingia ikulu ya Zanzibar katika kipindi cha miaka mitano ijayo.


Raia EAC ruksa kuajiriwa Tanzania
TANZANIA imefungua milango ya ajira mbalimbali zikiwamo za ualimu na uuguzi kwa ajili ya raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) chini ya Soko la Pamoja linaloanza kutekelezwa rasmi leo.

Nchi nyingine wanachama ni Uganda, Kenya, Rwanda, na Burundi ambazo pia zimeainisha ajira ambazo hazitakuwa na vikwazo kwa raia wa nchi mwanachama kuzipata katika nchi husika.

"Raia wa nchi wanachama wataruhusiwa kutafuta ajira katika maeneo yaliyofunguliwa katika nchi mwanachama yeyote na kutobaguliwa kwa misingi ya utaifa, katika masuala ya ajira na maslahi na haki nyingine za mfanyakazi," amesema Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax.

Ajira zilizofunguliwa na Tanzania kwenye sekta binafsi kwa nchi wanachama bila kubanwa na sheria ya kazi inayokataza kuajiri wageni kwenye maeneo ambayo watanzania wanamudu, ni pamoja na ualimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, maofisa ugani, wauguzi na wakunga, waongoza ndege, wahandisi wa fani mbalimbali na upimaji ramani.

Akifafanua jana maeneo ya msingi yaliyoondolewa vikwazo chini ya itifaki ya Soko la Pamoja, Tax alisema walimu wa vyuo vikuu wanaoruhusiwa kuanzia sasa kufanya kazi nchini ni wenye Shahada za Uzamivu.

Walimu wa sekondari walioruhusiwa ni wenye Shahada katika masomo ya Sayansi, Hisabati na lugha za kigeni na utekelezaji wake umepangwa kuanza mwaka 2015.

Kwa upande wa shule za msingi, kuanzia mwaka huu wanaruhusiwa walimu wa kutoka nchi wanachama wenye shahada za kwanza na wengine wanaoruhusiwa kuingia nchini kuanzia mwaka huu ni wa kilimo, ufundi stadi na utamaduni.

Ajira nyingine zilizoruhusiwa wageni kutoka nchi wanachama kuzipata na mwaka wa utekelezaji kwenye mabano ni maofisa ugani (2015), wauguzi na wakunga (2010), waongoza ndege (2012) na upimaji ramani (2015).

Kwa upande wa Kenya, miongoni mwa ajira zilizofunguliwa ni za utawala na uongozi, utaalamu katika masuala ya Sayansi, Hisabati, kompyuta, takwimu, Uhandisi na elimu maalumu.

Ajira nyingine ni kwa walimu wa shule za msingi na elimu ya juu, waongoza ndege, mawakili na maofisa wa sheria, wandishi wa habari, wafamasia, wauguzi, wasanii wa katuni, uchoraji na sanaa ya muziki.

Nchini Uganda, chini ya Soko hilo, raia wa nchi yoyote mwanachama, hana kikwazo cha kwenda kufanya kazi za uandishi wa habari, umakamu mkuu wa chuo kikuu, usanii, uanamuziki na uongozaji ndege.

Burundi imeweka wazi ajira za walimu wa vyuo vikuu, wauguzi na wakunga na wanataaluma wa Fizikia, Hisabati na Sayansi ya uhandisi kwa wageni kutoka nchi wanachama wa EAC.

Miongoni mwa ajira zilizofunguliwa Rwanda kwa ajili ya wageni ni za wataalamu wa Sayansi ya Jamii, Uhandisi, Upima ardhi, Utawala na Ualimu.

Akizungumzia uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuingia katika nchi yoyote ndani ya Jumuiya, Tax alisema raia atawajibika kuwa na hati halali ya kusafiria na kupita katika vituo rasmi mipakani, ambako baada ya kukamilisha taratibu za Uhamiaji, atapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa miezi sita.

Hata hivyo habari kutoka Rwanda zilisema nchi zote za EAC isipokuwa Tanzania, zimeruhusu matumizi ya vitambulisho vya kitaifa kama hati halali za kusafiria. Tanzania iko katika maandalizi ya kuchapisha vitambulisho hivyo.

Kwa upande wa matumizi ya ardhi na majengo, Ibara ya 15 ya Itifaki, inasema suala hilo litasimamiwa ndani ya nchi mwanachama na sheria za nchi husika.

"Hili la ardhi ni miongoni mwa masuala yaliyoibua hisia, watu wakadhani wageni wangekuja kuchukua ardhi. Lakini tumelinda maslahi ya Tanzania, wakija wageni watawezeshwa kupata maeneo ya biashara ila wataongozwa na sheria zetu za uwekezaji na ardhi," alisema Tax.

Majadiliano ya Itifaki ya kuanzisha Soko la Pamoja yalikamilika Oktoba mwaka jana na kufuatiwa na marais wa nchi wanachama, kuisaini Novemba 20 mwaka jana mjini Arusha.

 


War crimes court agrees to call Naomi Campbell

A war crimes court has ruled that model Naomi Campbell can be called to testify in a case against former Liberian President Charles Taylor.

Prosecutors for the UN-backed court for Sierra Leone say she was given a "blood diamond" by Mr Taylor in 1997 at Nelson Mandela's house in South Africa.

Mr Taylor is accused of using such diamonds to fuel an insurgency in Sierra Leone that cost many lives.

Ms Campbell had previously refused to provide testimony to prosecutors.

The Special Court for Sierra Leone, sitting in The Hague, also agreed to a prosecution request that it be allowed to call actress Mia Farrow and Ms Campbell's former agent Carole White to testify.

Ms Farrow - who was also at the Mandela dinner - has said Ms Campbell told her about the gift of the diamond the morning after the dinner.

Ms Campbell said she had been visited by representatives of Mr Taylor during the night, and that they had given her a "huge" uncut diamond, Ms Farrow told ABC News in April.

CHARLES TAYLOR

Charles Taylor in The Hague
  • 1997: Elected Liberian president
  • 2003: Arrest warrant issued, steps down, goes into exile in Nigeria
  • 2006: Arrested, sent to Sierra Leone
  • 2007: Trial opens in The Hague
Profile: Charles Taylor Q&A: Trying Charles Taylor

Ms Farrow and Ms White were both willing to testify, the prosecutors' request to the court said.

Mr Taylor is accused of selling diamonds and buying weapons for Sierra Leone's Revolutionary United Front (RUF) rebels, who were notorious for hacking off the hands and legs of civilians during the brutal 1991-2001 civil war.

He has pleaded not guilty to 11 counts of war crimes and crimes against humanity stemming from the war.

He has also dismissed the claims he presented Ms Campbell with a diamond in 1997.

"Blood diamonds" is the name given to diamonds mined in areas of conflict that are sold to fund warfare.

Mr Taylor's trial opened in June 2007.

In their request to subpoena the three women, the prosecutors said they did not know about the alleged Campbell diamond until June 2009, by which time they had already closed their case.

Mr Taylor had sought to prevent their bid to reopen the case against him. Defence witnesses are now being heard.